Wednesday, September 21, 2011

Mashairi Mtaani

Today I would like to dedicate my acknowledgements to one great champ by the name Victor Kabane who resides in Eastlands in Nairobi. Victor has the love and passion for poetry, I like his profile when he says; "I use my words to best describe that which is ethical to share to the rest of the world. I never calculate my words, i like it when i say it all..." I was inspired with is creativity after listening to one of his poems at a graduation ceremony last month. So for more about him check http://mywordsinblood.blogspot.com/

Kiswahili poem by Victor Kabane. Revieved via e-mail

SAFARI

Safari tuliianza, mwishoni hatujafika
Hivi sasa twajikaza, safari itakamilika
Wazazi twawapongeza, kutuelimisha mumewajibika
Ni mbali tulikotoka, safari tutaikamilisha

Wazazi manyumbani, nidhamu tumepata
Waalimu shuleni, elimu mwatupa
Wahubiri makanisani, kumcha Mungu mwatufunza
Ni mbali tulikotoka, safari tutaikamilisha

Sana twawashukuru, kwa kutuongoza safarini
Sisi mumetunusuru, hatujaingia taabani
Maulana hatutozi ushuru, kwenye safari yu uongozini
Ni mbali tulikotoka, safari tutaikamilisha

Leo hii twafurahia, maneno haya twayazungumzia
Ni ya kweli twawaambia, yote hayo mmeyasikia
Maneno hayajatuishia, ni mengi tungewaambia
Ni mbali tulikotoka, safari tutaikamilisha

No comments:

Post a Comment